Video duration: 102 seconds
Global video hits: 3453
Waziri mkuu Raila Odinga kwa mara nyingine tena amerejelea umuhimu wa kuachiliwa kwa washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi. Raila ana maoni kuwa amani haitorejea iwapo polisi ambao anashtumu wataendelea kushikilia washukiwa hao bila mashtaka yafaayo. Raila amedokeza kuwa ni kupitia tume ya Waki ambapo maswala kama hayo ya baada ya uchaguzi yanafaa yajadiliwe.
Video duration: 133 seconds
Global video hits: 527
Waziri wa Sheria na Katiba Martha Karua amesema kujiuzulu kwa makamishna wa tume ya uchaguzi nchini ECK hakutasaidia lolote iwapo miundo msingi ya uchaguzi na shughuli za kisiasa haitobadilishwa. Karua alisema udanganyifu kwenye uchaguzi unatokana na upungufu katika miundo msingi ya uchaguzi na shughuli za vyama vya kisiasa.
Video duration: 109 seconds
Global video hits: 2568
Mkuu wa Sheria Amos Wako amesema hakuna mashtaka yeyote yaliyofunguliwa dhidi ya washukiwa wa ghasia za kisiasa kufuatia upelelezi duni katika idara ya polisi. Wako aliyekuwa akitoa ushahidi mbele ya tume ya Waki, vilevile alielezea zaidi ya washukiwa na mashahidi 1000 wa ghasia za baada ya uchaguzi wako mafichoni hivyo basi kutatiza shughuli za kuwashtaki washukiwa.
Kijana kutoka kibera anawahimiza watu hasa vijana wasiuze kura zao. Pia anawahimiza watu kuishi pamoja kwa amani hata ingawa wan maoni tofauti ya kisiasa. [Man from Kibera encourage youth not to sell there votes. Also calls for peaceful coexistance between people who support different parties.]
Video duration: 177 seconds
Global video hits: 216
Kenya ingali inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi yaliyosababishwa na machafuko baada ya uchaguzi uliopita.
Pia, mabadiliko ya kiuchumi duniani, hasa katika soko la mafuta, yanachangia baadhi ya matatizo yanayokabili Kenya. Ni katika muktadha huu ndio tunaona bei ya kila kitu ikipanda na kuwaacha wengi hoi wasijue watazitoa wapi pesa za kuyakidhi mahitaji yao ya kimsingi.